Kila mtoto hizaliwa na uwezo wa pekee sana kimwili na kiakili. Lakini uwezo huo huathiriwa na vitu vingi ikiwemo mazingira na watu wanao mzunguka, ambao humjengea tabia ambazo anaishi nazo katika maisha yake. Tabia hizo zinaweza kubadilika kulingana na mazingira pia aina ya watu anao kutana nao katika makuzi yake. Aina ya watu wanaomzunguka wanaweza kia chanzo Cha kuharibu au kufifiza kipaji na ubunifu wa mtoto.
Zifuatazo ni mbinu za kukuza ubunifu wa mtu.
- Mruhusu mtoto akutane na changamoto. Hii ni njia nzuri kumfanya ajifunze mambo mengi ya msingi kupitia changamoto. Njia hii itamfanya ajue namna ya kujipambia bila kumtemea mtu moja kwa moja, itamfanya abuni mbinu ya kutoka kwenye changamoto.
- Mpatie uhuru na punguza kumkosoa kwa Kila kitu anacho Fanya. Watoto wanao banwa hawezi kufikiria vizuri na kupambana na mambo yanayo wazunguka kwa upana. Mpatie fulsa ya kufanya vitu kwa vitendo.
- Mpatie vifaa changamshi. Mpatie vifaa ambavyo havija kamilika. Mfano mnunulie toi la gari haru toa tairi ndio umpatie aunganishe mwenyewe.
- Mpatie fursa ya kufikiria. Mpatie mtoto nafasi ya kukupinga katika baadhi ya mambo na sikiliza mawazo na maoni yake. Wakati mwingne fanyia kazi maoni yake. Hii itamfanya awe na uwezo wa kufikiria tofauti na wengine.
Njia zilizo tajwa hapo juu zitamfanya mtoto awe na uwezo na ubunifu mzuri katika makuzi yake.
0 comments: