Sunday, August 18, 2024

NAMNA YA KUKABILIANA NA UKOSEFU WA AJIRA (SEHEMU YA KWANZA). Karibu tujifunze ujasiriamali kwa mtaji usiozidi TSH 100,000/=




UJASIRIAMALI NI NINI?

Ujasiriamali ni mchakato wa kuunda, kuanzisha, na kusimamia biashara ili kuzalisha faida. Kupitia ujasiriamali, watu huchukua hatari na kutumia ubunifu ili kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii, kuunda ajira, na kuendeleza uchumi. Nchini Tanzania Kuna tatizo la ajira kwa vijana kutokana na idadi kubwa ya vijana wanaingia kwenye soko la ajira Kila mwaka wakiwa na maarifa na ujuzi mbali mbali unaohijika katika jamii. Lakini tukumbuke siku zote fursa hua zina ukomobau ni chache lakini mahitaji ya ajira ni makubwa hivyo serikali na sekta binafsi haziwezi kutoa ajira kwa Kila mmoja. Inakadiliwa kua vijana 1,000,000 wanaingia wanaingia kwenye soko la ajira Kila mwaka lakini vijana 200,000 pekee ndio wanaopata ajira Kila mwaka. Hivyo Kila mwaka Kuna vijana 800, 000 wanaongezeka kwenye soko la ajira bila mafanikio ya kupata ajira.

NINI KIFANYIKE VIJANA WAPATE AJIRA?

Suruhisho la tatizo la ajira ni Ujasiriamali. Kama vijana wote wataweza kutumia maarifa na ujuzi walio nao kujitenhenea ajira wenyewe, basi tatizo la ajira nchini litapungua kwa kiasi kikubwa. 

Fanya yafuatayo kuondokana na tatizo la ajira. 

  • Ubunifu.
  • Ukarbu na watu sahihi.
  • Mawazo chanya.
LEO TUTAJIFUNZA NAMNA YA  KUTENGENEZA SABUNI YA VIPANDE.



MALIGHAFI
  • Kostiki soda
  • Maji safi
  • Mafuta ya mise/arizeti
  • Sodium silicate 
  • Chumvi lakini
  • Box la kugandishia
  • Perfume na rangi (sio lazima)


HATUA ZA UTENGENEZAJI.
  • Chukua ndoo tupu safi
  • Weka maji 350mls
  • Weka kostiki soda vijiko 6 na kologa kwa dk 2.
  • Acha ipoe kwa masaa 12 au zaidi. Na baada ya kupoa, 
  • weka chumvi vijiko 2 ili igande mapema na kologa Hadi chumvi iyeyuke.
  • Weka perfume na rangi na kologa kwa dk 2 Hadi 5. Hakikisha rangi imechanganyika vizuri.
  • Mimina kwenye box la kugandishia kwa masaa 12 Hadi 18.



0 comments: